TRADUIRE LE CONTENU DU BLOG

lundi 2 janvier 2012

MOT DE REMERCIEMENT EN KISWAHILI DE LA SOEUR BEATA, PROVINCIALE DES CMT A MATANDA


Leo ni siku ya furaha kubwa katika Eklezya nzima na kwa upekee katika shirika la mabikira Wakarmelita Missionari wa Mtakatifu Tereza wa Avila. Leo tunasherehekea yubileo ya miaka 200 ya kuzaliwa kwa Mwenye heri Francisco Palau y Quer, mwanzishi wa shirika letu. Kwa tarehe ya leo, 29/12/1811, Padri Francisco Palau alikuwa akizaliwa huko Espania mjini Aitona.
Mwaka wa 1861 alianzisha shirika letu la Mabikira wakarmelita Misionari wa Mtakatifu Tereza.
  Tarehe 20/03/1872 alifariki pa Tarragona – Espania.

Upendo huo ambao Francisco Palau alikuwa nao kwa Eklezya ndio sisi mabinti wake tulirizi. Uwito wa mabikira wakarmelita ni uwito wa kusali na kupenda Eklezya. Kupitia vitendo na kazi mbambali wanayofanya duniani kote, wanatangazia watu Uzuri wa Eklezya na kuwaalika pia kupenda na kutumikia Eklezya kwa moyo wote. Wakarmelita wanaishi kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya Eklezya: Kazi wanazofanya ni kwaajili ya kutuliza vidonda vyenye kuisumbua.
Kazi hiyo tunaifanya katika dunia nzima. Hapa Afrika, tunaeneza enjili ya mapendo katika inchi 7: RDC, Rwanda, Kenya, Cameroun, Senegal, Mali na Madagascar.

Tuna sababu nyingi za kushuru Mungu kwa siku ya leo.

1.              Leo tunawapasha kama mama mkubwa wa Roma  alikubali ombi la mabikira wa provincia ya Afrika, ya kuanza upya kazi ya kitume katika parokia ya Matanda.  Shauri kuu la Provincia la Afika huko Nairobi limetuma mabikira wane kwa kufungua upya nyumba ya Matanda: Mama Aurelie Bulambo (mama mkubwa wa communaute), mama Anastasie Kahasha, mama Georgette Bisimwa na mama Olive Nabuholwe. Mabikira watatu watatumika katika kituo cha afia (=centre de sante) na 1 atatumika Shule.
 
Baada ya kuwahimiza mukaribishe viruzi mabikira na watoto wenu, ninataka kusema: AKSANTI SANA. NINASHUKURU :

1.      Mungu kwa kuwa amekamilisha mpango wa kutukusanyisha hapa ili tugawanye furaha ya yubileo hii kama jamaa moja

2.      Baba Askofu, Theofile KABOY kwa jina la Mere Générale, la mabikira wote na langu binafsi. Tunampigia aksanti kwa kukubali tufungue upya nyumba hii ya Matanda ambayo ilifungwa karibu myaka 16. Pia kwa sababu aliitika ombi letu la kufungia mwaka huu wa yubileo katika jimbo lake na kwa upekee katika parokia ya Kristu Mfalme ya Matanda, iliyokuwa makao ya kwanza ya viongozi wetu hapa Afrika.

3.      Tunamshukuru pia Askofu mustaafu Faustino Ngabu aliyetuhimiza kila mara kuanza tena utumishi katika parokia hii na parokia zingine za jimbo la Goma. Tunamuombea baraka nyingi katika kazi yake ya kitume.

4.      Padri Innocent NYIRINDEKWE: tunakushukuru kwa kuwa umeitika kusimamia sherehe hii ukisoma misa ya shangwe. Ufikishe shukrani zetu kwa Akina Baba Askofu aliyetamani kuwa nasi leo lakini hakuweza sababu ya vizuiyo mbalimbali vya kazi yake ya uchungaji.

5.      Tunashukuru Padri mkubwa wa Parokia ya Matanda na mapadri wasaidizi wake waliojitolea sana kwa kutupokea leo. Tunashukuru pia mapadri wote waliojiunga nasi kwa sherehe hii.

6.      Shukrani zetu pia kwa mabikira wote  waliohapa na kwa namna ya upekee wa Carmelites wa Goma, wa postulantes, wa aspirantes na wa MILPA, kwa kujitolea kwa  matayarisho ya sherehe hii na waliotusaidia kwa namna mbalimbali.

7.      Tunashukuru pia wa dada wamisionari wetu wa kwanza walioanza shirika la wa Carmelites hapa Matanda na kwa namna ya upekee dada Gema Miro aliye kati yetu. Yeye ndiye alianza hili shule la msinji la wasichana, EP Kitumaini.

8.      Tunasema pia asante kwa watawa wote, marafiki na jamaa waliotoka Goma, Bukavu, Rwanda na kazalika ili wajiunge nasi leo,

9.      Viongozi wa Serkali na wa majeshi nao wapokee shukrani zetu kwa kulinda usalama wa watu wote na kwa kufanya siku ya leo ipite katika amani.

10.  Shukrani zetu ziwafikie waimbaji kwa nyimbo nzuri na sauti nyororo. Walitusaidia kusali na kuchangamusha sherehe hii.

11.  Siwasahau vikundi mbalimbali vilivyo tayarisha mahali hii tunapokaa; wale wamama wanaopika jikoni, wababa na wavijana wote waliosaidia kwa kazi mbalimbali za kuandaa sikukuu hii

Nanyi wakristu wote wa matanda kwa jumla mubarikiwe sana kwa kuwa mumeacha kazi zenu mbali mbali kwa kuja kukusanyika nasi katika sala. Kupitia sherehe hii, Mungu awape nguvu na imani ili muwe mashahidi wa mapendo na amani yake kati ya watu.

Kwa yote, Tunashukuru. Mubarikiwe sana.

IMEFANYIKA MATANDA TAREHE 29/12/2011
Sœur  Beata KAYITESI SIMBIZI
Supérieure Provinciale

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire